#Local News

WAITITU ANYIMWA DHAMANA NA MAHAKAMA

Ni pigo kwa gavana wa zamani wa Kiambu Ferdinand Waititu baada ya ombi lake la kutaka aachiwe huru kwa dhamana akisubiri rufaa yake ya kupinga hukumu dhidi yake kutupiliwa mbali kwa misingi kwamba hajawasilisha sababu za kuishawishi mahakama impe dhamana hiyo.

Miongoni mwa sababu alizotoa kutaka dhamana ni kuhusu afya yake, sababu ambayo mahakama imepinga ikisema hospitali za magereza zina vifaa vya kutosha na kwamba endapo kuna dharura basi mfungwa anaweza kuwasilishwa katika hospitali ya rufaa.

Aidha, mahakama imemhakikishia kuwa rufaa yake itasikilizwa kwa haraka ndani ya kipindi cha miezi 2.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WAITITU ANYIMWA DHAMANA NA MAHAKAMA

HISIA ZA SHA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *