#Local News

UTULIVU WAREJEA MAJENGO NAIROBI

Utulivu umeanza kureja katika eneo la Majengo karibu na soko la Gikomba jijini Nairobi kufuatia makabiliano mapema leo kati ya polisi na kundi la vijana lililozua vurugu kulalamikia mauaji ya kijana mmoja, wanayesema alipigwa risasi na polisi wa kituo cha California kufuatia tofauti kati ya polisi na kundi la watu wanaosemekana kuwa wauzaji wa mihadarati.

Gari la polisi na afisi ya chifu ni miongoni mwa mali ambayo imeteketezwa kwenye vurugu hizo, vijana hao wakiibua madai kwamba wamekuwa wakidhulumiwa na polisi mara kwa mara.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *