AFISA ‘ALIYEUAWA’ MAJENGO AFUTWA KAZI, POLISI

Afisa wa polisi anayedaiwa kufyetua risasi na kusababisha kifo cha mvulana mwenye umri wa miaka 17 mtaani Majengo jijini Nairobi amepokonywa bunduki na kusimamishwa kazi huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
Haya ni kwa mujibu wa msemaji wa idara ya polisi Michael Muchiri, ambaye amewataka wenyeji kushirikiana na maafisa wa idara DCI na kitengo cha kushughulikia masuala ya ndani kwa ndani wanaofanya uchunguzi.
Aidha, amewataka wenyeji hasa vijana, kudumisha utulivu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa