WAHUDUMU WA UHC WAENDELEZA MGOMO NORTHRIFT
Huduma za matibabu katika vituo mbali mbali vya afya kwenye kaunti zote 7 za Northrift zimeendelea kusambaratika kufuatia mgomo unaoendelea wa wahudumu wa afya walioajiriwa chini ya mpango wa afya kwa wote UHC, ambao wamekongamana mjini Kapsabet kaunti ya Nandi kufanya maandamano.
Wahudumu hao wanashinikiza kuajiriwa kwa kanadarasi ya kudumu, wakidai kwamba serikali imewapuuza.
Wameapa kutorejea kazini hadi malalamishi yao yatakaposhughulikiwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































