IEBC KUANZA MAHOJIANO YA MWENYEKITI NA MAKAMISHNA LEO

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) inaanza mahojiano ya kujaza nafasi ya mwenyekiti na makamishna sita, mchakato wa siku 33 utakaoanza leo Jumatatu jijini Nairobi.
Kamati ya uteuzi inayoongozwa na Dr. Nelson Makanda itaendesha mahojiano haya kwa awamu, ambapo wagombea 11 wa nafasi ya mwenyekiti watahojiwa kati ya Machi 24 na 26, kisha wagombea 105 wa makamishna kati ya Machi 26 na Aprili 24.
Tume mpya itakabiliana na changamoto za uadilifu wa uchaguzi na uhakiki wa sajili ya wapiga kura, ikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa 2027.
Imetayarishwa na Janice Marete