MZIGO WA WAFANYIKAZI HEWA WAMLEMEA MLIPA USHURU

Mkenya mlipa ushuru ameendelea kuathirika baada ya tume ya utumishi wa umma (PSC) kugundua wafanyikazi hewa 17,000 wanaogharimu serikali mabilioni ya fedha kila mwaka.
Waziri wa utumishi wa umma, Justin Muturi, amewasilisha mswada wa 2024 wa usimamizi na maendeleo ya utumishi wa umma, unaolenga kuondoa wafanyikazi hewa, kufanya ukaguzi wa mishahara kila robo mwaka, na kuimarisha usimamizi wa pensheni na bima ya matibabu kwa watumishi wa serikali.
Imetayarishwa na Mercy Asami