#Local News

MAKATIBU WAKUU WATEULE KUHOJIWA APRILI

Wakenya 14 walioteuliwa na Rais William Ruto maajuzi kuwa makatibu wakuu katika wizara mbali mbali watahojiwa na kamati husika za bunge la kitaifa tarehe 4 na tarehe 7 Aprili ili kubaini uwezo wao wa kuhudumu kwenye nyadhifa hizo.

Kupitia tangazo, karani wa bunge hilo Samuel Njoroge amesema tayari spika Moses Wetang’ula amezifahamisha kamati hizo.

Miongoni mwa teuzi hizo ni Ouma Oluga ambaye atafika mbele ya kamati ya afya, Judith Pareno akifika mbele ya kamati ya haki na masuala ya kikataiba na Ceryll Wagunda ambaye atahojiwa na kamati ya fedha.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MAKATIBU WAKUU WATEULE KUHOJIWA APRILI

WAKENYA HUKOPA MILIONI 500 KILA SIKU, RIPOTI

MAKATIBU WAKUU WATEULE KUHOJIWA APRILI

WANYAMA AJIUNGA NA ATHLETIC FC

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *