MICHEZO YA SEKONDARI KUANZA RASMI LEO MOMBASA

Hatua Kitaifa ya Muhula wa Kwanza Michezo ya Shule za Sekondari ya Kenya (KSSSA) 2025, zimepangwa kuanza hii leo huku mabingwa wa kanda wakikutana Mombasa kwa wiki moja ya mashindano makali.
Kuanzia leo hadi Aprili 12, Mombasa itakuwa kitovu cha michezo ya shule za upili, huku Shule ya Upili ya Wavulana ya Shimo la Tewa, Shule ya Upili ya Wasichana ya Mama Ngina, Chuo cha Ualimu cha Shanzu, na Aga Khan Academy, zote zikishiriki michezo hiyo iliyojaa shughuli nyingi.
Katibu Mkuu wa KSSSA Pwani, McDonald Dzile, aliwahakikishia washiriki wote kwamba Mombasa iko tayari kutandaza zulia jekundu.
Edwin Morara, kocha wa raga katika Shule ya Kisii, pia anapania kuwaondoa mabingwa watetezi wa raga, All Saints.
Michezo hiyo itaanza kwa hafla rasmi ya ufunguzi katika Chuo cha Ualimu cha Shanzu kutayarisha mafunzo ya siku ya Jumanne asubuhi.
Imetayarishwa na Nelson Andati