LIVERPOOL WAENDELEZA MAZUNGUMZO NA SALAH

Liverpool wanaendelea na mazungumzo ya kumpa mkataba mpya Mohamed Salah huku viongozi hao wa Premier League wakizidi kuamini kwamba atasalia Anfield msimu ujao.
Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri mwenye umri wa miaka 32 unamalizika mwishoni mwa msimu huu pamoja na wachezaji wenzake wa Liverpool Virgil van Dijk na Trent Alexander-Arnold.
Wakati Alexander-Arnold akihusishwa sana na uhamisho wa bila malipo kwenda Real Madrid, Van Dijk alisema baada ya kupoteza kwa mabao 3-2 Jumapili dhidi ya Fulham kwamba mazungumzo yanaendelea kuhusu mkataba mpya.
Salah ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu huu akiwa amefunga mabao 27 na amefunga mabao 243 katika mechi 394 akiwa na Reds tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Roma mwaka 2017.
Imetayarishwa na Nelson Andati