#Business

BUNGE LA KENYA LAPENDEKEZA KUBADILISHWA KWA SEHEMU YA 19 YA SHERIA YA AJIRA

Wabunge wamemtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuifuta au kuirekebisha Sehemu ya 19 ya Sheria ya Ajira ya mwaka 2007, ambayo inazuia makato ya mshahara kuwa zaidi ya theluthi mbili ya malipo ya msingi ya mfanyakazi.

Pendekezo hili linakuja kutokana na kuongezeka kwa makato ya kisheria kama vile Ada ya Makazi, Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii (SHIF), na michango ya NSSF, ambayo imeshusha kiwango cha mshahara kinachobaki kwa watumishi wengi wa umma hadi chini ya asilimia 30.

Kamati ya uhasibu imemuagiza waziri wa fedha kutafuta ushauri wa kisheria kuhusu jinsi ya kuainisha sheria hiyo na makato ya sasa.

Imetayarishwa na Mercy Asami

BUNGE LA KENYA LAPENDEKEZA KUBADILISHWA KWA SEHEMU YA 19 YA SHERIA YA AJIRA

WAMATANGI, WENGINE 8 MASHAKANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *