TAHADHARI YA KIPINDUPINDU: WATU 6 WAFARIKI

Wakenya wametakiwa kuchukua tahadhari kufuatia mlipuko wa kipindupindu ambao tayari umeua watu sita na kuwaathiri wengine 100 katika maeneo mbalimbali nchini.
Msemaji wa serikali Isaac Mwaura amesema serikali inachukua hatua kuhakikisha ugonjwa huo unadhibitiwa, huku akisisitiza umuhimu wa usafi wa mazingira na matumizi ya maji safi ili kuzuia maambukizi zaidi.
Imetayarishwa na Janice Marete