SHUGHULI ZAVURUGIKA KWENYE KIWANDA CHA NZOIA KUFUATIA MAANDAMANO
Shughuli katika kiwanda cha sukari cha Nzoia zimetatizika baada ya wafanyakazi kuandamana kupinga ubinafsishaji wa kiwanda hicho.
Wafanyikazi hao aidha wanasema kuwa hawatakubali usimamizi mpya kabla ya kulipwa mishahara yao yote, wakidai serikali inapuuza maslahi yao na sheria za ajira licha ya huduma yao ya muda mrefu.
Inaarifiwa kuwa tayari serikali imekamilisha mchakato wa kubinafsisha kiwanda hicho
Imetayarishwa na Janice Marete
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































