SERIKALI YAKARIRI SHARTI ILIPWE

Serikali imesema inafanya kila iwezalo kuhakikisha wakopaji wote wa fedha kutoka hazina ya Hustler Fund wanalipa mikopo hiyo ili kuhakikisha hazina hiyo inawainua kiuchumi wakenya.
Akizungumza mbele ya seneti, waziri wa mashirika na biashara ndogo ndogo na vya kadri Wycliffe Oparanya, amesema kufikia sasa shilingi bilioni 70 zimekopwa na wakenya milioni 25.
Kufikia Oktoba mwaka jana, shilingi bilioni 12 zilizokopwa hazikuwa zimerejeshwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa