BOLGNA WAWAPIKU AC MILAN
Wachezaji wa Bologna wamemaliza kiu chao cha miaka 51 cha Kombe la Italia baada ya
kuchukua ushindi wa bao 1 dhidi ya AC Milan mjini Rome.
Kocha mkuu wa klabu hiyo, Vincenzo Italiano, aliyechukua usukani kutoka kwa Thiago
Motta, ameonyesha juhudi zake kwa kuleta utofauti wa historia hii iliyoanza kunakiliwa mwa
wa 1974 tangu kuanzishwa kwa mashindano ya kombe hilo mwaka wa 1964.
Dan Ndoye alifunga bao hilo lililowavisha taji, katika kipindi cha pili dakika ya 53.
Ikumbukwe kwamba Bologna hawajawahi kushiriki kwenye fainali tangu ushindi wao wa
mwisho.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































