MARAGA NCHINI TANZANIA KUSHUHUDIA KESI YA TUNDU LISSU

Jaji Mkuu mstaafu David Maraga amewasili Tanzania kushuhudia kesi ya Tundu Lissu, kiongozi wa chama cha upinzani Chadema.
Hii ni baada ya Martha Karua, Gloria Kimani na Lynn Ngugi kuzuiwa kuingia nchini humo na kurejeshwa Kenya.
Lissu anakabiliwa na mashtaka ya uhaini kutokana na hotuba ya kuhamasisha uasi kabla ya uchaguzi wa 2025. Chama chake kiliondolewa kwenye uchaguzi huo mwezi Aprili.
Imetayarishwa na Janice Marete