MGONJWA AJINYONGA HOMA BAY, UCHUNGUZI WAANZA

Uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha kifo cha mgonjwa anayedaiwa kujinyonga katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Homa Bay
Marehemu, kwa jina Mike Juma, anaripotiwa kujinyonga ndani ya choo cha wodi alipokuwa akipata matibabu baada ya kulazwa kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa Polisi marehemu alikuwa ameacha kutumia dawa za TB kabla ya tukio hilo. Mwili umehifadhiwa kwenye hifathi ya maiti ya hospitali hiyo ukisubiri uchunguzi zaidi.
Imetayarishwa na Janice Marete