#Local News

WANAHARAKATI WASHINIKIZA NJERI AACHILIWE

Huenda shughuli za biashara zikatatizika hii leo jijini Nairobi kutokana na maandamano ya wanaharakati ambao wametangaza kuandamana ili kushinikiza kuachiwa huru kwa mwenzao Rose Njeri aliyekamatwa Ijumaa iliyopita na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Pangani.

Njeri alikamatwa baada ya kutengeneza tovuti inayowawezesha wakenya kupinga mswada wa fedha wa mwaka wa 2025/26, huku juhudi za wanaharakati kutaka apewe dhamana ya polisi kufeli licha ya taarifa kwamba ana matatizo ya kiafya.

Kupitia tovuti hiyo, wakenya wanawezeshwa kuwatumia wabunge pingamizi rasmi kwa urahisi kuhusu vifungu vyenye utata.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WANAHARAKATI WASHINIKIZA NJERI AACHILIWE

SHA YA POLE POLE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *