VIHIGA QUEENS WAPIGIWA UPATO KUSHINDA KOMBE LA FKF

Kocha mkuu Boniface NyamuNyamu alisema ni lazima Vihiga Queens itimize katika Kombe la FKF msimu huu ambao umekua mgumu sana.
Mabingwa mara nne wa Ligi Kuu ya Wanawake watamenyana na Bungoma Queens katika nusu-fainali siku ya Jumapili, na Nyamu anatazamia kuelekea fainali huku wakilenga kukwepa kampeni nyingine isiyo na taji.
Mchezo huu utaandaliwa katika uwanja wa Mumias Sports Complex huku timu ya Kenya Police Bullets itakayochuana na Kibera Soccer Women katika nusu-fainali nyingine uwanjani Dandora siku hiyohiyo.
Vihiga Queens ilimaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi huku Bullets wakifanikiwa kuhifadhi taji lao kwa pointi 43, mbili juu ya Ulinzi Starlets walio nafasi ya pili.
Vihiga Queens waliwazaba Eldoret Falcons 4-1 katika mikwaju ya baada ya mechi na kufuzu kwa nusu fainali huku Bungoma Queens waliwazaba Trinity Queens 3-0 katika robo fainali ya Kenya Police Bullets waliwazaba Zetech Sparks 3-0 katika robo fainali huku Kibera wakifuzu kwa nusu-fainali na washindi watatu wa Kombe la Star-4 kwa kuwafunga washindi 3 wa Star Cup
Imetayarishwa na Nelson Andati