#Sports

HARRIET OKACH ATEULIWA KUA MWENYEKITI WA KRU

Harriet Okach ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Raga nchini (KRU), na kuwa mwanamke wa kwanza kabisa kushikilia wadhifa huo katika historia ya shirikisho hilo.

Uteuzi wake ulithibitishwa Alhamisi, kufuatia kujiuzulu kwa Alexander ‘Sasha’ Mutai wiki jana.

Katika hotuba yake ya kwanza baada ya uteuzi huo, Okach aliahidi kuwaleta washikadau wote pamoja kwa ajili ya ukuaji wa mchezo huo.Kabla ya uteuzi wake, Okach alikuwa mwanachama wa bodi ya KRU, akisimamia Masoko na Biashara.

Zamani alikuwa mweka hazina wa Kisumu RFC kabla ya kujiunga na KRU kama mwanachama wa bodi mnamo 2023.

Aliyekuwa Mwenyekiti Mutai alijiuzulu Ijumaa wiki jana kwenye mkutano mkuu maalum (SGM) uliokuwa na dhoruba katika uwanja wa RFUEA, kabla ya pendekezo la kutokua na imani naye na vilabu wanachama.

Okach atahudumu kwa muda uliosalia hadi uchaguzi mpya ufanyike.

Imetayarishwa na Nelson Andati

HARRIET OKACH ATEULIWA KUA MWENYEKITI WA KRU

KAULI YA VIONGOZI WA KALENJIN TRANS NZOIA

HARRIET OKACH ATEULIWA KUA MWENYEKITI WA KRU

BINGWA WA MBIO ZA PARIS CHEBET ANASEMA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *