#Local News

KAULI YA VIONGOZI WA KALENJIN TRANS NZOIA

Viongozi wa jamii ya Kalenjin katika kaunti ya Trans Nzoia wameikosoa serikali kwa madai ya kumhangaisha kisiasa gavana wa kaunti hiyo George Natembeya na maafisa wengine wa serikali yake waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Wakiongozwa na Eliud Tormoi, viongozi hao wamesema serikali inalenga kumdhalilisha gavana huyo, wakitoa wito kwa taasisi za serikali kutekeleza majukumu yao bila kuingiliwa kisiasa.

Aidha, wamewaonya viongozi kutoka nje dhidi ya kuingilia uongozi wa kaunti hiyo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KAULI YA VIONGOZI WA KALENJIN TRANS NZOIA

AJIRA YA CLIMATE WORX

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *