#Sports

KOCHA WA KABATI FC AHAKIKISHA KUA AMEJITOLEA KUANDIKISHA HISTORIA

Kocha mkuu wa Kabati Youth FC Joe Mungai amethibitisha kujitolea kwake kwa timu hiyo yenye maskani yake Murang’a kufuatia kupandishwa kwao kihistoria hadi Ligi ya daraja la pili nchini (NSL).

Mungai alifichua kuwa licha ya kupokea ofa kutoka kwa timu za Ligi Kuu ya FKF, amechagua kusalia na Kabati Youth na kuiongoza klabu hiyo katika kampeni yake ya kwanza ya NSL.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo Paul Mwangi alikiri kwamba kupandishwa daraja, ingawa ni baraka, kunakuja na kuongezeka kwa matatizo ya kifedha. Alibainisha kuwa klabu hiyo sasa inahitaji KSh. 15 milioni – kutoka KSh. milioni 12 – ili kukidhi mahitaji yake kwa msimu ujao.

Mmoja wa wachezaji mashuhuri wa timu hiyo, beki Amos Odhiambo, pia anatumai kuongeza muda wake wa kuichezea timu hiyo.

Imetayarishwa na Nelson Andati

KOCHA WA KABATI FC AHAKIKISHA KUA AMEJITOLEA KUANDIKISHA HISTORIA

YAMAL NA WILLIAM WANG’ARA

KOCHA WA KABATI FC AHAKIKISHA KUA AMEJITOLEA KUANDIKISHA HISTORIA

NAOMI OSAKA AJIONDOA KWA MASHINDANO YA QUEEN

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *