MAKAMANDA KUWAJIBIKIA UFISADI WA MAAFISA WAO

Makamanda wa polisi kote nchini watabebeshwa msalaba wa maafisa fisadi walio chini yao, ikiwa ni njia moja ya idara ya polisi kujisafisha kutokana na tope la ufisadi ambalo limeiandama kwa miaka.
Agizo hilo limetolewa na inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja, baada ya kikao na makamanda hao jijini Nairobi, akiwaagiza kuunda kamati za kuzuia ufisadi mbali na kuwasilisha ripoti kwake kila baada ya miezi 4.
Jukumu la kamati hizo litahusisha kuchunguza visa vyote vya ufisadi miongoni mwa maafisa walio chini yake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa