NDOTO YA IRAN KUSHUUHUDIA KOMBE LA DUNIA YADIDIMIA

Mashabiki wa soka wa Iran wanatazama ndoto yao ya kushihudia Kombe la Dunia ikitoweka baada ya marufuku ya kusafiri ya Marekani kuwazuia kuingia katika taifa Hilo kuishangilia timu yao.
Michuano hiyo ya 2026 itaandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada na Mexico, lakini mechi nyingi, ikiwemo fainali, zimepangwa kuchezwa katika ardhi ya Marekani.
Wengi nchini Iran walikuwa wameng’ang’ania matumaini ya kushangilia timu Yao kwenye viwanjani vya Marekani hadi jana wakati Rais wa Marekani Donald Trump alipoweka marufuku mpya ya kusafiri kwa nchi 12 ikiwemo Iran, ambayo itaanza kutekelezwa kuanzia Jumatatu.
Marufuku hiyo haitawahusu wachezaji watakaoshiriki katika michuano ya Kombe la Dunia la 2026 au Olimpiki ya Los Angeles 2028, lakini mashabiki wao wamepigwa marufuku, huku uhusiano wa kidiplomasia ukivunjika kati ya mataifa hayo mawili tangu mapinduzi ya Kiislamu ya 1979.
Imetayarishwa na Nelson Andati