EMUSIRE BOYS NDIO MABINGWA VIHIGA
Shule ya upili ya Emusire Boys ndio mabingwa wa kandanda katika kaunti ya Vihiga baada ya kuwabandua Ebwali kwa mabao 2:1 katika mechi ya aina yake iliyochezwa kwenye uwanja wa Chavakali High Jumamosi.
Emusire wanaotoka eneo bunge la Emuhaya, walifaidi kutokana na makosa kwenye safu ya ulinzi ya Ebwali na kufunga bao la kwanza kupitia kwa Vincent Achono kufuatia shambulizi la kushtukiza, kabla ya Alloy Peter kufuta uongozi wao na kufanya mambo kuwa sawa.
Hata hivyo, Wayne Okindo alihakikisha Emusuire wanatawazwa washindi kunako dakika ya 78 baada ya kupiga shuti la kichwa kutokana na mkwaju wa kona.
Kwingineko, Madira Girls walitawazwa washindi kufuatia ushindi mwembamba wa bao 1:0 dhidi ya Ibubi.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































