TAALAM, MUKHWANA WATAKA KESI YAO ISITISHWE
OCS wa kituo cha Central jijini Nairobi Samson Taalam na afisa mwingine wa polisi anayehudumu katika kiuo hicho James Mukhwana waliokamatwa kuhusiana na mauaji ya bloga Albert Ojwang, wamewasilisha ombi mahakamani wakitaka kesi dhidi yao isitishwe.
Kupitia kwa wakili wao Danstan Omari, maafisa hao wanasema kwamba kukamatwa kwao na maafisa wa mamlaka ya IPOA kulifanyika mapema bila uchunguzi na kukumbwa na dosari, na kukariri kuwa uchunguzi ni muhimu ufanyike kabla ya kesi ya uhalifu kuanza.
Wameshikilia kuwa iwapo utaratibu hitajika hautafuatwa basi huenda kesi hiyo ikahujumiwa.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































