VITUO VYA POLISI KUWEKWA CCTV
Vituo vyote vya polisi 1209 vitawekwa kamera za cctv katika muda wa miaka 2 ijayo ili kuimarisha utendakazi na kuhakikisha uwazi katika shughuli zinazoendeshwa.
Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen anasema watawasilisha bungeni pendekezo la kutaka kuharamishwa kitendo chochote cha kuhitilafiana na kamera hizo.
Anasema hitilafu yoyote katika mitambo hiyo inastahili kuripotiwa katika muda wa saa moja ili hatua za haraka zichukuliwe.
Imetayrishwa na Maureen Makhobe
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































