HELB YAWASAKA WAKOPAJI WALIOKWEPA

Imebainika kuwa idadi kubwa ya wakenya waliokopa fedha za ufadhili wa masomo ya juu kutoka kwa bodi ya mikopo HELB haijarejesha fedha hizo, HELB ikisema inawadai wakenya hao takribani shilingi bilioni 40 zilizokopwa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Kwenye mahojiano na runinga moja nchini, afisa mkuu mtendaji wa HELB Geoffrey Monari, amesema bodi hiyo inawalenga wanafunzi hasa waliofuzu katika kipindi cha mwaka 1 na 11 iliyopita warejeshe fedha hizo.
Kulingana naye, wanafunzi waliosomea taaluma ya ualimu wamekuwa wakijizatiti kulipia mikopo yao.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa