MMOJA APOTEZA MAISHA KWENYE MAANDAMANO

Mtu mmoja amepoteza maisha kwenye maandamano yaliyoshuhudiwa hapa Nairobi baada ya kukabiliwa na polisi kwenye barabara ya Moi.
Kulingana na video inayoendelea kusambazwa mitandaoni marehemu ambaye alikuwa akiendelea na biashara yake ya kuuza maski alivamiwa na polisi 2 waliompiga kabla ya mmoja kumfyatulia risasi na kisha kuondoka.
Watu wengine wanaendelea kuuguza majeraha na wengine kuzuiliwa na polisi.
Imetayrishwa na Maureen Mukhobe
‘