#Local News

MADEREVA, BODA BODA KUKAZA KAMBA CHINI YA SHERIA MPYA

Waendesha boda boda na madereva wa magari ya umma wanaojihusisha ukiukaji wa kanuni za barabarani watalazimika kukaza mkanda baada ya wabunge kuidhinisha mswada wa fedha 2025 ambao una sheria na kanuni zilizochapishwa na Waziri wa uchukuzi nchini Davis Chirchir zinazowalenga ili kuleta mabadiliko na ubora katika sekta ya uchukuzi.

Baadhi ya sheria alizopendekeza Waziri ni Pamoja na sheria ya upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kupitia chombo cha alcoblow, sheria nyingine ni ile ya ukaguzi wa magari na sheria ya viwango wa usalama kwa magari ya shule ikiwa ni Pamoja na mikanda ya usalama na vifaa vya kuzima moto.

Hapo awali, Waziri huyo alibainisha kuwa sheria hizo mpya zitakuwa na adhabu ya hadi shilingi 100,000, ikiwa dereva atapatikana akiwa mlevi, mbali na leseni yake kufutiliwa mbali

Imetayrishwa na Antony Nyonesa

MADEREVA, BODA BODA KUKAZA KAMBA CHINI YA SHERIA MPYA

MAHAKAMA YAWAPA WANAUME AFUENI

MADEREVA, BODA BODA KUKAZA KAMBA CHINI YA SHERIA MPYA

AFISA WA POLISI MUKHWANA RUMANDE SIKU 21

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *