#Local News

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YA MWANAHARAKATI NJERI

Ni afueni kwa mwanaharakati Rose Njeri aliyekamatwa baada ya kutengeza tovuti ya kuwawezesha wakenya kutoa maoni yao kuhusu mswada wa fedha, baada ya mahakama kutupilia mbali kesi dhidi yake.

Kwenye uamuzi wake, hakimu mwandamizi wa mahakama ya Milimani Geoffrey Onsaringo, amesema stakabadhi zilizowasilishwa mahakamani zilikosa kuafikia viwango hitajika kwa kesi kuendelea.

Njeri aliyetuhumiwa kwa makosa ya kukiuka sheria kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii, amekuwa huru kwa dhamana ya shilingi elfu 100.

Imetayrishwa na Antony Nyonesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *