MSWADA WA FEDHA: KIPENGEE TATA CHATEMWA

Wakenya wanaolipa ushuru wamepata afueni baada ya kipengee chenye utata kilicholenga kuipa nguvu mamlaka ya kukusanya ushuru KRA kufikia deta zao bila idhini yao au ya mahakama kuondolewa kwenye mswada wa fedha wa mwaka wa 2025-26.
Kipengee hicho kilichozua shutuma dhidi ya KRA, kililenga kuiruhusu mamlaka hiyo kufikia maelezo ya kibinafsi ya walipa ushuru ikiwemo taarifa zao za benki na simu za mkononi ili kudhibiti ukwepaji kulipa kodi.
Mswada huo uliopitishwa hapo jana, utawasilishwa kwa Rais ili kutiwa saini na kuwa sheria ya fedha ya mwaka ujao wa kifedha.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa