GACHAGUA: SERIKALI INAFADHILI WAHUNI

Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua ambaye pia ni kinara wa chama cha DCP,amemshutumu Rais William Ruto kwa madai kwamba anafadhili makundi ya wahuni kuendeleza vurugu dhidi ya viongozi wa upinzani nchini akiwemo Gachagua mwenyewe.
Akizungumza kwenye kaunti ya Meru, Gachagua amedai kuwa serikali imekuwa ikifadhili makundi ya wahuni kuwakabili wanaofanya maandamano ya amani, na kuitaka kuwalinda kikamilifu watakaoshiriki maandamano yaliyopangwa kufanyika Jumatano wiki hii.
Kauli yake imesisitizwa na mwenzake wa Wiper Kalonzo Musyoka.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa