#Local News

HOFU YAENDELEA MWIKI KUHUSU MAUAJI

Wakazi wa mwiki eneo bunge la Kasarani jijini Nairobi wameendelea kulalamikia visa vya utovu wa usalama na madai ya polisi kutumia nguvu kupita kiasi, baada ya mwenzao kwa jina Joshua Stephen mwenye umri wa miaka 18 kudaiwa kupigwa risasi na afisa wa polisi wakazi walipokuwa wakiandamana kulalamikia mauaji ya Abigael Wanjiku mwenye umri wa miaka 21 nyumbani kwao.

Kanda za CCTV zinawaonyesha maafisa 7 wa polisi wakishika doria eneo hilo siku ya Jumamosi, kabla ya mmoja wao kumfyetulia risasi kijana huyo, mamlaka ya IPOA sasa ikisema itachunguza tukio hilo.

Wakiongozwa na mbunge wa eneo hilo Ronald Karauri, wakazi wamewataka polisi kuuimarisha usalama.

Imetayrishwa na Antony Nyongesa

HOFU YAENDELEA MWIKI KUHUSU MAUAJI

WETANG’ULA AHIMIZA KANISA KUOMBEA NCHI

HOFU YAENDELEA MWIKI KUHUSU MAUAJI

SAKAJA AJITENGA NA UHUNI NAIROBI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *