!6 WAFARIKI KUTOKANA NA MAANDAMANO- AMNESTY

Ripoti zimeonyesha ongezeko la idadi ya watu walioafariki kutokana na maandamano ya hapo jana, ripoti za hivi punde zikiweka idadi hiyo kuwa watu 16, wengi wao wakiuawa na maafisa wa polisi.
Mkurugenzi wa shirika la Amnesty Internationla Irungu Houghton, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba idadi hiyo imethibitishwa na mashirika kadhaa, akisema waathiriwa 5 walipigwa risasi na kufariki papo hapo.
Hata hivyo, msemaji wa polisi Muchiri Nyaga, amedinda kuzungumzia ripoti ya shirika hilo.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa