BIASHARA ZAKADIRIA HASARA YA MAMILIONI NAIROBI
Wafanyabiashara kadhaa katikati mwa jiji la Nairobi wanaendelea kukadiria hasara ya mamilioni ya pesa baada ya biashara zao kuporwa wakati wa maandamano ya hapo jana.
Maeneo yaliyoathirika pakubwa na OTC, Bus Station nae neo la Koja ambako pia wanawake kadhaa waliokuwa wakijiandaa kusafiri kwenda Qatar kusaka ajira, walinusurika kifo baada ya jengo walimokuwa kushika moto katika eneo hilo la Koja.
Mabaki ya vioo na majivu yangali taswira ya jiji.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































