RANGERS WASALIA KWA LIGI KUU

Posta Rangers wamehifadhi nafasi yao ya Ligi Kuu ya FKF (FKFPL) licha ya kupokea kichapo cha 1-0 kutoka kwa Naivas FC katika mkondo wa pili wa mchujo wa kupanda daraja/kushuka daraja uliochezwa mjini Murang’a.
Wanabarua hao walishikilia faida ya jumla ya 2-1, baada ya kupata ushindi wa 2-0 katika mkondo wa kwanza mjini Thika wikendi iliyopita.
Imetayarishwa na Nelson Andati