#Local News

BLOGA ALBERT OJWANG KUZIKWA TAHARUKI IKITANDA

Mazishi ya bloga na mwalimu Albert Ojwang yameratibiwa kufanyika hii leo katika kijiji cha Kokwanyo kaunti ya Homa Bay huku taharuki ikiwa imetanda, baada ya waombolezaji kuvamia na kuteketeza kituo cha polisi cha Mawego ambako Ojwang aliwasilishwa mara ya kwanza alipokamatwa kabla ya kifo chake.

Waombelezaji hao wakiwemo wanafunzi wa chuo kimoja cha kiufundi eneo hilo, walivamia msafara na kuchukua mwili wa Ojwang’ kabla ya kuelekea nao kituoni humo na kuwalazimu maafisa wa polisi kukimbilia usalama wao baada ya makabiliano ya takribani saa 3.

Kulingana na kamanda wa polisi kaunti ya Homa Bay Lawrence Koilen, afisi ya OCS wa kituo hicho na rekodi zote za polisi kituoni ni miongoni mwa mali iliyoteketezwa

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *