MAANDAMANO: ODINGA APENDEKEZA KURA YA MAONI
Kinara wa ODM Raila Odinga amependekeza mazungumzo ya kitaifa kufanywa yakiwaleta Pamoja wadau kutoka vizazi tofauti, ili kutatua masuala yanayoibuliwa na vijana wa kizazi cha Gen Z ambayo sasa yametishia mshikamano wa nchi.
Akizungumza na wanahabari, Odinga amelalamikia changamoto zilizoko ikiwemo utendakazi wa polisi, licha ya maandamano ya Saba Saba ya mwaka 1990 kushinikiza mageuzi nchini.
Odinga aliyasema haya baada ya kukosa kufika katika uwanja wa Kamukunji kuahdimisha maandamano hayo jinsi alivyokuwa amepanga.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































