#Sports

OCHIENG AFURAHISHWA NA UCHEZAJI WA TIMU YAKE

Kocha mkuu wa Strathmore Blades Tony Ochieng amefurahishwa na uchezaji wa timu yake wikendi katika mechi za Ligi Kuu ya Kikapu ya Kitaifa ya Kenya baada ya kushinda moja na kupoteza nyingine.

Wanafunzi hao waliwashinda NBK Phoenix 70-55 kabla ya kuangukia 76-86 dhidi ya wenzao wa chuo kikuu cha UoN Terror wikendi. Wakati huo huo, Ochieng anaangazia mechi iliyosalia dhidi ya magwiji wa Mamlaka ya Bandari ya Kenya (KPA), akitumai kushinda, huku wakivuka vidole vyao kwa uwezekano wa kufuzu.

Imetayarishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *