#uncategorized

KITUO CHA POLISI CHACHOMWA NYAMIRA

Taharuki imetanda katika eneo la Bonyunyu kaunti ya Nyamira, baada ya wakazi wenye hasira kukiteketeza kituo cha polisi cha Itibo wakilalamikia kufyetuliwa risasi kwa mwanamme mwenye umri wa miaka 19 wakati wa makabiliano kati ya kundi la wanafunzi na polisi.

Polisi wamesema kituo hicho mwanzo kiliporwa kabla ya kuchomwa, ila wakathibitisha kuwa hakuna bunduki zilizopotea.

Makabiliano hayo yalizuka baada ya wanafunzi hao kuanza maandamano nje ya afisi ya mwakilishi wa wadi eneo hilo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KITUO CHA POLISI CHACHOMWA NYAMIRA

KARUA AMTAKA RUTO NJE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *