HESHIMU MAHAKAMA, KOOME AWAAMBIA WAKOSOAJI
Jaji mkuu Martha Koome amelalamikia uingiliaji wa shughuli za idara ya mahakama na mashambulizi dhidi ya maafisa wa idara hiyo, akisema mwelekeo huo utaathiri utoaji haki kwa umma.
Koome ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la kitaifa kuhusu haki, amewataka maafisa hao kusalia imara na kutekeleza majukumu yao bila upendeleo.
Haya yanajiri huku waziri wa usalama Kipchumba Murkomen akiikosoa idara hiyo kutokana na jinsi inavyoshughulikia kesi kuhusu washukiwa wa uharibifu wakati wa maandamano.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































