KANJA KUFIKA BUNGENI KUHUSU MGOGORO WA NPS-NPSC
Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja anatarajiwa kufika mbele ya bunge la kitaifa kutoa mwanga kuhusu mgogoro uliopo kati ya idara ya polisi NPS na tume inayosimamia raslimali ya polisi nchini c
Hii ni baada ya mkurugenzi mkuu wa tume hiyo, Peter Lelei kuwasilisha lalama akidai kwamba Kanja ameweka kimaksudi mikakati inayozuia tume hiyo kutekeleza wajibu wake.
Anadai kuwa Kanja amekataa kuwasilisha orodha ya malipo kwa ajili ya ukaguzi licha ya Lelei kuandaa kikao kilicholenga kuleta suluhu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































