MSHUKIWA MKUU WA MAUJAJI KNH AKAMATWA
Maafisa wa idara ya upelelezi DCI wamemkamata mshukiwa mkuu katika mauaji ya mgonjwa wa pili aliyepatikana akiwa ameuawa katika wodi ya wagonjwa kwenye hospitali ya kitaifa ya Kenyatta, ikiwa ni chini ya miezi 5 baada ya mgonjwa mwingine kuuawa katika wodi iyo hiyo.
Mgonjwa huyo wa kiume Edward Maingi mwenye umri wa miaka 54, alipatikana akiwa amelowa damu kitandani alikokuwa amelazwa, karibu na kitanda ambako Gilbert Kinyua mwenye umri wa miaka 39 alipatikana akiwa amekatwa koo mwezi Februari mwaka huu.
DCI imemtambua mshukiwa kuwa Kennedy Kalombotole, anayeendelea kuchunguzwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































