MUNYAKO APONEA HUKUMU, KUREJEA NCHINI
Familia ya Stephen Munyakho, mkenya aliyekuwa amehukumiwa kunyongwa nchini Saudi Arabia ina kila sababu ya kutabasamu, baada ya serikali kutangaza kwamba yuko huru na anatarajiwa kurejea nchini.
Ikiongozwa na mamake Dorothy Kweyu ambaye ni mwanahabari mkongwe, familia hiyo imetoa shukrani kwa mashirika yaliyofanikisha fedha za kulipa kama faini kwa familia ya mwathiriwa.
Munyakho alihukumiwa nchini Saudi Arabia mnamo mwaka wa 2011 baada ya kuhusika kwenye mapigano na raia mmoja wa Yemen na kusababisha kifo cha raia huyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































