MZOZO WA MIGINGO WAPATA MWAFAKA
Hatimaye mzozo wa miaka mingi kuhusu umiliki wa kisiwa cha Migingo kilichoko katika Ziwa Victoria umepata suluhu baada ya Rais William Ruto na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni kutia saini mkataba wa kumaliza mzozo huo.
Kwenye mkataba uliotiwa saini na wawili hao katika Ikulu ya Nairobi, kisiwa hicho cha Migingo kitatumiwa na Kenya na Uganda, hatua ambayo itawapa wavuvi matumaini ya kuendeleza shughuli zao ziwani humo bila hofu ya kuhangaishwa na vikosi vya usalama.
Aidha, wawili hao wametia saini mikataba mipya 8 kuhusu ushirikiano mbali mbali ukiwemo uvuvi na kilimo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































