#Sports

STARS WAKABA KOO ANGOLA

Timu ya Kenya Harambe Stars inaongoza jedwali la kundi A na alama 4 katika mashindano ya CHAN 2024 baada ya kupata sare ya bao 1-1 hapo jana katika mechi yenye ushindani mkubwa dhidi ya Angola katika uwanja wa Kasarani, Nairobi.

Angola ilitangulia kuongoza mechi hiyo kwa bao moja katika dakika ya 7 ya kipindi cha kwanza naye Austin Odhiambo wa Stars akajibu dakika 5 baadae kupitia kwa mkwaju wa penalti.

Aidha Stars walijikakamua kupata alama zote 3 licha ya mchezaji Marvin Omondi kupata kadi nyekundi katika dakika 21, kipindi cha kwanza, hali iliyowapelekea kucheza mechi ngumu zaidi iliyoisha kwa sare.

Furaha ya Angola ilionekana kukatizwa katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza walipofunga bao lakini likakatupiliwa mbali kupitia mfumo wa teknolojia ya VAR.

Morocco ambao wanatarajiwa kucheza jumapili dhidi ya Stars ndio nambari 2 kwenye jedwali na alama 3 wakifuatiwa na DRC Congo waliowacharaza Zambia mabao 2-0 kutoka kwa Japhte kitambala nan a Malanga Mwaku katika uwanaja wa Nyayo, Nairobi jana jioni.

Angola nao kwa sasa ni nambari 4 wakiwa na alama 1 huku Zambia ikifunga jedwali hilo la kundi A bila alama yoyote.

Imetayarishwa na Nelson Andati

STARS WAKABA KOO ANGOLA

MATIBABU YAFANYIWA MAGEUZI NCHINI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *