#Local News

UCHUNGUZI WAANZISHWA KWENYE MKASA WA NDEGE KIAMBU

Vikosi mbali mbali vya usalama vinanendeleza uchunguzi katika mkasa wa ndege ya shirika la Amref iliyoanguka hapo jana katika eneo la Mwihoko kaunti ya Kiambu, na kusababisha vifo vya watu 6.

Ndege hiyo ndogo iliyokuwa ikitoka uwanja mdogo wa ndege wa Wilson jijini Nairobi kuelekea Hergeisa nchini Somalia, iliangukia nyumba kadhaa mtaani humo muda mfupi baada ya kupaa angani.

Kamishna wa kaunti ya Kiambu Henry Wafula, amesema serikali itafanya uchunguzi wa kina kuibaini chanzo cha ajali hiyo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UCHUNGUZI WAANZISHWA KWENYE MKASA WA NDEGE KIAMBU

MATIBABU YAFANYIWA MAGEUZI NCHINI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *