#Local News

SERIKALI YA MACHAKOS TAYARI KUZUNGUMZA NA WAUGUZI

Huenda mgomo wa wauguzi ambao umeathiri huduma za matibabu katika kaunti ya Machakos ukapata suluhu baada ya serikali ya kaunti hiyo kujitolea kufanya mazungumzo na wauguzi wanaogoma.

Naibu gavana wa kaunti hiyo Francis Mwangangi amesema serikali hiyo itafanya kila iwezalo ili kumaliza mgogoro huo kwa lengo la kuwahakikishia wakazi huduma za matibabu.

Nao wauguzi hao wameitaka kaunti hiyo kuzingatia maelewano ya kuongezewa mshahara na hata kupandishwa vyeo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SERIKALI YA MACHAKOS TAYARI KUZUNGUMZA NA WAUGUZI

MWANAMME AMUUA NDUGUYE HOMABAY

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *