LYLES ABWAGWA
Jana usiku bingwa wa Olimpiki wa mbio za mita 100, Noah Lyles alichapwa tena na Oblique Seville wa Jamaika, ambaye aliibuka na ushindi kwa sekunde 9.87 kwenye pambano lililojaa mvua la mkondo wa Athletissima wa Diamond League huko Lausanne Uswisi.
Lyles alitumia sekunde 10.02 na kushindwa kwa mara ya tatu mfululizo katika maururu wa Ligi ya Diamond, wiki chache kabla ya kutetea taji lake la dunia mjini Tokyo.
Nyota huyo wa Marekani alisema alianza vibaya kabla ya kumkimbiza Ackeem Blake anayeanza kwa kasi – lakini alisisitiza kuwa atakuwa tayari kwa Tokyo.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































