HOSPITALI YAWAKATAA WAFUNGWA
Wafungwa wanaotegemea huduma za matibabu katika hospitali ya Mbagadhi jijini Nairobi wataendelea kukosa huduma hizo kwa wiki 3 sasa baada ya hospitali hiyo kusitisha huduma za matibabu kwa wafungwa kutokana na deni la zaidi shilingi milioni 12.
Kupitia notisi, usimamizi wa hospitali hiyo umesema idara ya magereza haijalipa malimbikizi hayo kutokana na huduma za matibabu zilizotolewa kwa wafungwa kwa kipindi cha miaka kadhaa.
Kulingana na hospitali hiyo, imefanya kila iwezalo ili kulipwa kwa deni hilo ila idara hiyo bado imesalia kimya.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































